Friday, July 30, 2010

TANZANITE SOCIETY JPSauti ya Mwanamke a.k.a Asma Kobayashi kugombea nafasi ya Naibu katibu Mkuu
Asma Kobayashi wa kwanza kushoto


Nimefikiria kwa muda, na kuonelea kuwa huu ni wakati muafaka wa kujitolea kuitumikia Jumuia yetu kwa nafasi ya NAIBU KATIBU MKUU hivyo naomba unipatie FORM ya kugombea uongozi katika nafasi hiyo ili niweze kuwawakilisha wanawake wenzangu katika Jumuia yetu kwa karibu zaidi.

Pia napenda kuchukuwa nafasi hii kuwaomba wanawake wenzangu waishio Japan kujitokeza kwa wingi siku hii ya uchaguzi tarehe 1/8/2010 ikiwa ni pamoja na maombi ya kunipa kura zao. Bila kuwasahau Kaka zangu ambao ndio wengi wetu hapa Japan pia naombeni kura zenu

No comments: