Thursday, July 01, 2010

TANZANITE SOCIETY JP

TANGAZO LA UCHAGUZI
WA VIONGOZI WA JUMUIYA
YA WATANZANIA WANAOISHI JAPANI
Kamati ya uchaguzi wa viongozi wa jumuiya ya watanzania wanaoishi Japani inapenda kuuwatangazia wanajumuia wote kuwa UCHAGUZI wa VIONGOZI wapya wa jumuia utafanyika JUMAPILI, TAREHE 01/ 08 / 2010 katika ukumbi wa ODASAGA PLAZA-Odakyu Sagamihara Station kuanzia SAA 11.45 jioni. Tume inawakaribisha wale wote wenye SIFA wanaopenda kuongoza jumuia yetu kwa kipindi cha MIAKA MIWILI.

Sifa za mgombea:
1. Awe na umri usiopungua miaka 18.
2. Awe mkazi, wenye anuani na namba ya simu
3. Awe mwanachama HAI na amelipa ada ya uanachama hadi mwezi wa 8 mwaka huu.
4. Alipie ADA ya kuomba kugombea
a. Nafasi ya mwenyekiti wa jumuiya Yen 5000/-
b. Nafasi zingine Yen 3000/-

Nafasi zilizo wazi:
1. Mwenyekiti wa jumuiya
2. Makamu mwwnyekiti wa jumuia
3. Katibu wa jumuiya
4. Naibu katibu wa jumuia
5. Mweka hazina
6. Makamu wa mweka hazina


Kamati inawaomba wale wote wenye sifa na wanaopenda kugombea nafasi hizo wawasiliane na wana kamati wafuatao:

1. Mwenyekiti kamati ya uchaguzi bw Amani Paul - 080 4200 0684
2. Katibu wa kamati ya uchaguzi bw Kamugusha - 090 8581 9202
3. Wajumbe wa kamati ya uchaguzi:
i. Mama Mariam Nyangasi (Mama Joe) 080 3413 4942
ii. Miss Pendo – 080-1326 9700
iii. Mr Amarilo
iv. Mr Ngereza – 090-9845 9699

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu ibariki jumuia yetu, Mungu wabariki wanachama wa jumuia wanaoishi Japani.

By,
Paul Amani
Mwenyekiti wa kamati.
28/06/2010

1 comment:

chib said...

Kila la heri katika uchaguzi wa viongozi wenu