Saturday, June 26, 2010

TANZANITE SOCIETY JP

WORLD CUP

Wanatija mpo?? naona huku ukumbini watu wamekata tamaa kabisa na Team za Africa.

Je mmeona Ghana alivyomtoa Mmarekani kwa kumcharanga 2-1 mbele ya Bill Clinton wao na wengineo. Ghana inatutoa aibu lazima tuwe wazalendo GHANA YEEEEEEEEEEE! !

Samahanini kwani sauti imenikauka kwani shamrashamra za jana usiku zilikuwa babu kubwa kwani niliweza kuangalia mpira huu LIVE katika maeneo ya Ebisu Tokyo kulikuwa na wamarekani kama 6 na sisi wafrika tulikuwa 4 wajapan 12 ukumbi ulikuwa umeenea mbwembwe za wamarekani lakini cha kushangaza wajapan walikuwa wanashangilia Ghana. "eeh eeh ghana suyoi suyoi samorai ghana, samorai ghana eeeeyeeeeeeee" .

Huku wamerekani wakitujibu kwa kututishia kuwa America big nation yeeeey usa, usa, usa yeeee.

Yes!!!!!! mcheza kwao hutunzwa, dispelling America 2-1 yeeee Ghana kiboko yao.
"MIND YOU AFRICA IS THE MOTHER LAND".

Wako,
Sauti ya Mwanamke (Asmah Kobayashi)

No comments: