Thursday, June 03, 2010

TAARIFA YA KISOMO CHA MAMA WA BW. RAJABU UREMBO‏

Ndugu Watanzania wenzangu,

Kwa heshima napenda kuwataarifu kuwa kisomo cha marehemu Zainabu binti Pazi, mama mzazi wa Bw. Rajabu Urembo kitafanyika siku ya tarehe 6/6/2010 (Jumapili) katika ukumbi wa Tsuruma kuanzia saa 8 mchana mpaka saa 11 jioni. Muda huu unatokana na ukumbi kutumika na watu wengine katika masaa mengine yaliyobaki.

Tafadhali tunaomba wahudhuriaji kufika ukumbini angalau 7:45, kufika kwetu kwa muda kutasaidia kukamilisha shughuli hii mapema kwani tutatakiwa kupanga na kusafisha ukumbi kwa ajili ya watumiaji wengine watakaoingia saa 11.

Ahsanteni sana

Simba
Mwenyekiti, Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Nchini Japani