Tuesday, April 27, 2010

TANZANITE SOCIETY JP

Taarifa ya msiba

Ndugu wanatija na watanzania wenzangu,Uongozi wa jumuiya ya Tanzanite Society umepokea taarifa kuwa mwanajumuiya mwenzetu Dada Sabina Itambiko amefiwa na Dada yake mpendwa Bi. Ida Itambiko kule nyumbani Tanzania.Marehemu alifariki akiwa amelazwa kwenye hospitali ya Muhimbili siku ya Ijumaa 23 Aprili na kuzikwa siku ya Jumapili 25 Aprili kwenye makaburi ya Kinondoni.Kama kawaida yetu naomba tuungane pamoja kumfariji dada yetu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na maombolezo. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Bi. Ida Itambiko mahali pema peponi. Amen.Shughuli ya ibada ya kumuombea marehemu hapa Japani itafanyika siku ya Jumapili tarehe 2/5/2010. Taarifa zaidi zitatolewa baadae.

Senkoro.
Katibu mkuu msaidizi.

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

pole kwa msiba tuwombee marehemu kwa njia ya sala. Marehemu astarehe kwa amani peponi amina.