Saturday, December 12, 2009

Tanzanite Society JP


Mkutano wa Jumuiya ya Watanzania Japani wafana

Jumuiya ya Watanzania Wanaoish nchini Japani (TANZANITE SOCIETY) leo Jumapili tarehe 6 Disemba walifanya mkutano wao wa mwisho wa mwaka ambako masuala muhimu kuhusiana na Jumuiya yalijadiliwa. Ajenda kuu ya mkutano huo pamoja na mambo mengine ilihusisha wanachama kupatiwa taarifa mbalimbali za maendeleo ya Jumuiya ikiwa ni pamoja na hatua iliyofikiwa katika kusajili Jumuiya kuwa NGO, kujadili na kutathmini zoezi la ulipaji ada kwa Wanajumuiyapamoja na suala muhimu la kujadili na kuamua kuhusu kuweka utaratibu wa kusaidia wenye shida nyumbani Tanzania.
Wajumbe walijitokeza kwa wingi kuhudhuria mkutano huo na kuchangia katika mijadala mbalimbali. Wamepongeza uongozi kwa kufanikisha zoezi la kusajili rasmi Jumuiya kuwa NGO na kuwaomba waongeze jitihada katika kuhamasisha kupata wanachama wengi zaidi na ukusanyaji wa ada. Blogu ya Wananchi inachukua fursa hii kupongeza uongozi wa Tanzanite na wanajumuiya kwa jitihada zao zilizofanikisha kufikisha Jumiya katika hatua hii nzuri.
Chini ni baadhi ya picha zilizopatikana katika mkutano huo.