Monday, December 28, 2009

Sherehe Mwaka Mpya

Sherehe za kuukaribisha Mwaka Mpya 2010 Tokyo
Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Nchini Japani (Tanzanite Society) inapenda kuchukuwa fursa hii kuwatangazia Watanzania wote wa Kanto na maeneo ya jirani na wale watakaokuwa wanatembelea Kanto wakati huu wa kipindi hiki cha Mwaka mpya joto kuwa kutakuwa na sherehe kabambe ya kuukaribisha mwaka mpya (2010). Sherehe hizi zitafanyika huko Mkoani Kanagawa. Maelezo kamili ya shughuli hiyo ni kama ifuatavyo:-

Siku: 3/1/2010 (Jumapili)
Muda: Kuanzia saa tatu usiku mpaka majogoo
Kiingilio: Yeni 1500 (utapata kinywaji kimoja)
Ukumbi: Amore Club uliopo ghorofa ya pili ya jengo la Grande Hon Asugi, Hon Asugi, Nakacho-2-13-13, ilipofanyikia sherehe ya Uwataja2008 (Karibu na ukumbi wa mama Mperu). Dakika 5 toka kituo cha train cha Hon Asugi (Odakyu line)

Muziki: DJ mkongwe, DJ Zee atakupatia miziki ya aina mbalimbali kuanzia zile za kizazi cha zamani (enzi za mababu zetu) mpaka za kizazi cha kipya, hip hop, taarab, nk.

Kwa ufafanuzi na maelekezo ya ziada tafadhali wasiliana na wanakamati wa kamati ya Uhamasishaji na Starehe:
Bw Pembe: 080-3458-8786
Bi Angela: 080-3397-0339
Bi Upendo: 080-1326-9700
Bi Mariam: 090-4422-8555
Bw Ntale: 080-4149-1257

Tunawaomba watanzania pamoja na marafiki zao wa mataifa mengine kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha shughuli hii. Ukipata taarifa hii mtaarifu na mwenzio.

Ahsanteni
Kwa niaba ya Kamati ya Uhamasishaji na Starehe
Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Nchini Japani

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Nawatakieni sherehe njema na pia mafanikio mema katika kuuanza mwaka 2010.