Sunday, October 11, 2009

DISCO LA HARAMBEEDisco na Harambee ya Kuwachangia Bw Abuu Omary na Bi Tatu Bwela‏

Ndugu Watanzania wenzangu, kama mnakumbuka vyema watanzania wenzetu Bw Abuu Omari na Bi Tatu Bwela walipata janga la kuunguliwa na nyumba yao takribani wiki mbili zilizopita. Kwa kuzingatia maadili yetu ya Kitanzania ya kusaidiana wakati wa matatizo, Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Nchini Japani (Tanzanite Society) inapenda kuwatangazia Disco la harambee, ili kuwachangia ndugu zetu hawa.

Disco hilo litafanyika siku ya JUMAPILI ya Tarehe 11 Mwezi wa 10 katika ukumbi wa SAGAMINO TROPICAN PUB kuanzia SAA TATU usiku. Ukumbi upo karibu na kituo cha train cha Sagamino (Sotetsu line)

Kiingilio kitakuwa Yen 1,500. Kwa wale watakaotaka kuchangia zaidi siku hiyo kutakutakuwa na Daftari la Michango ukumbini. Mapato ya Disko hili watakabidhiwa Bw Abuu na Bi Tatu.

Kwa wale wenzetu wasio weza kufika siku hiyo na wanapenda kuwasaidia watanzania hawa wanaweza kuwasilisha michango yao kwa kiongozi yeyote yule wa Jumuiya au kutuma mchango wake kwenye akaunti ya Jumuiya ilipo hapo chini:

ACC. NAME: Tanzanite Society
REPRESENTATIVE: Simba Ally Yahaya
ACC No.: 7916169
BRANCH NAME: Kunitachi
BRANCH No.: 666
BANK NAME: Mistui Sumitomo

Kwa wale watakaotaka maelezo zaidi tafadhali wasiliana na

Mwenyekiti: 090-3899-0638
Katibu: 090-4130-4754
Kamati ya starehe: 080-3458-8786

Ahsanteni na karibuni wote

Simba
Mwenyekiti
Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Nchini Japani.No comments: