Source: jamboafrica3.com
Monday, February 29, 2016
Tingatinga Art
Monday, February 22, 2016
Saturday, January 23, 2016
Saturday, September 26, 2015
Monday, September 14, 2015
Sunday, August 16, 2015
Monday, August 03, 2015
KILA LA HERI BINTI YETU ZAHARA KWENYE KURA ZA MAONI ZA UBUNGE WA CCMVIJANA MKOANI TAB
wa TBN Ughaibuni
Nyota njema huonekana asubuhi. Bila shaka umewahi kusikia msemo huu. Kwa Zahara Muhidini Issa Michuzi, nyota yake njema ni tunu ya uongozi. Tangu alipoweza kutambua maana na tofauti ya jambo jema na baya, amekuwa kiongozi.
Muhtasari wa maisha yake unaonyesha alizaliwa mnano tarehe 2 Septemba mwaka 1987 Nzega mkoani Tabora. Amesomea katika shule zifuatazo;
*Shule Ya Msingi Rufita, Tabora- 1995-2001
*Shule Ya Sekondari Kazima, Tabora-2002-2005
*Shule Ya Sekondari Ya Juu Emma, Kampala-Uganda 2007-2009
*Chuo Kikuu Cha Dodoma, Dodoma,Tanzania 2011-2014.
Zahara Muhidini Issa Michuzi, ambaye ni binti wa Ankal, ni mhitimu wa Shahada ya Sanaa katika masuala ya Uchumi. Mpaka kufikia hapa alipo, nyota yake ya uongozi imejidhihirisha katika sehemu mbalimbali alizopitia hususani shule.
Amekuwa kiranja, msimamizi wa shughuli na miradi mbalimbali shuleni na alipokuwa Chuo Kikuu Dodoma alikuwa kiongozi katika Jumuiya ya Wanafunzi- University of Dodoma Students Organization (UDOSO) akiwa kama Mbunge wa Baraza La Wanafunzi.
Mbali ya uzoefu wa kiuongozi alionao, Zahara anazo sifa zifuatazo ambazo ni nadra na tunu kubwa katika uongozi;
Anajitambua- Zahara anajitambua vilivyo. Anatambua kwamba uongozi ni heshima na utumishi uliotukuka.
Ana Ari Ya Kuongoza na
Kujifunza- Zahara anaamini kwamba kiongozi bora lazima awe ana ari ya kuongoza na kutumikia wananchi anaowaongoza. Mbali ya kuongoza,kiongozi lazima awe tayari kujifunza kutokana na hali halisi na kukabiliana na mabadiliko ya aina yoyote yanayoweza kujitokeza.
Ni Msikivu Na Ana uwezo Mkubwa wa Kufanya Kazi na Watu- Hili Zahara amelithibitisha katika ngazi zote za kiuongozi ambazo amepitia. Usikivu wake umekuwa chachu ya kumwezesha kutatua matatizo mbalimbali ambayo amekabiliana nayo huku yeye kama kiongozi akitarajiwa kuyatatua.
Ana Uwezo Wa Kuongoza Mabadiliko Ya Kijamii- Zahara anaamini kwa vitendo kwamba jamii yoyote lazima isonge mbele ili kwenda sambamba na mabadiliko mbalimbali ya kijamii. Anaamini kwa vitendo kwamba uongozi thabiti unahitajika ili kuleta mabadiliko chanya ambayo jamii yoyote inahitaji.
Zahara Muhidini Issa Michuzi hivi sasa anagombea kuwa mwakilishi wa vijana Bungeni kupitia Viti Maalumu Vijana (Youth Seats) kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM)- Tabora. Anaomba Kura na Ushirikiano Wako.
Wednesday, July 29, 2015
Tuesday, July 21, 2015
NGOMA AFRICA BAND KUTUMBUIZA INTERN.AFRICAN FESTIVAL TUBINGEN ,JUMAMOSI25 JULAI 2015
Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa Band aka FFU-Ughaibuni yenye makao yake nchini Ujerumani,inatarajiwa kutingisha jukwaa la
maonyesho makubwa ya muziki na utamaduni barani ulaya 6th International African Festival in Tübingen, Ujerumani, bendi hiyo maarufu inayoongozwa na Kamanda Ras Makunja itapanda jukwaani siku ya Jumamosi 27 Julai 2015majira saa 2.00 Usiku katika
uwanja wa Festplatz,Europa str,mjini Tübingen ,uliopo Ujerumani ya Kusini.
Kikosi kazi hiko cha Ngoma Africa Band ukipenda waite viumbe wa ajabu Anunnaki au FFU,chenye utajiri wa wanamuziki vijana waliojaa vipaji, bendi inasadikiwa kuwanasa
washabiki kila kona duniani kutokana na mdundo wake "Bongo Dansi" made in Uswahilini. bendi hiyo kwa sasa inatamba na CD mpya ya " La Mgambo" yenye nyimbo mbili za kumuaga rais JK
Saturday, July 18, 2015
ZAHRA MICHUZI KUWANIA UBUNGE VITI MAALUM (VIJANA) TABORA
Zahra Muhidin Michuzi akiweka sahihi katika kitabu cha wageni alipowasili katika ofisi za CCM mkoani Tabora ili kuchukuwa form ya kugombea ubunge viti maalum kwa vijana.
Binti huyo wa Michuzi baada ya kuhutimu elimu yake ya shahada ya uchumi UDOM ameona ni vyema akawatumikia wananchi wa nymbani kwake Mkoani Tabora kwa kutangaza nia ya kugombea ubunge wa viti maalum kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi
Diamond Platnumz Ft Mr Flavour - Nana
MAGUFULI NDIYE MGOMBEA URAIS WA CCM 2015
MBUNGE wa Biharamulo Mashariki (CCM) na Waziri wa Ujenzi, Mhe. John Pombe Magufuli ameshinda katika uchaguzi wa kumpata mgombea urais wa CCM kwa mwaka 2015. Magufuli ameshinda baada ya kupata jumla ya kura 2104 sawa na 87.1%, Balozi Amina Salum Ali amepata kura 253 sawa na 10.5% na Dk. Asha-Rose Migiro 59 sawa na 2.4%.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Makinda ndiye aliyepewa jukumu la kusoma mshindi katika kura za Kikao cha Mkutano Mkuu wa CCM kilichofanyika kuanzia jana na kuendelea leo asubuhi mkoani Dodoma.
Thursday, July 16, 2015
Subscribe to:
Posts (Atom)













































